Ajali Basi la NBS na Gari Dogo Yaua Watano Shinyanga

WATU watano wamefariki dunia papo hapo katika ajali iliyohusisha gari ndogo lililogongana na basi  la Kampuni ya NBS katika kijiji cha Nyasamba wilaya ya Kishapu mkoani Shinyanga barabara ya Shinyanga – Mwanza jana Alhamisi, Agosti 27, 2020.

Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga ACP Debora Magiligimba ambaye amefika eneo la tukio amesema chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo aina ya Toyota Secced kukosa mwelekeo na kugonga basi aina ya TATA, mali ya Kampuni ya NBS lililokuwa likitoka jijini Mwanza kuelekea mkoani Tabora.

 

“Gari lenye namba za usajili T571 BPZ aina ya Tata Mini Bus ikiendeshwa na Kazimili Maganga likitokea Mwanza kwenda Tabora lilipofika eneo la Nyasamba liligongana na gari jingine dogo likitokea Dar es Salaam likiendeshwa na Ramadhan Silaji na kusababisha vifo vya watu watano,” ameeleza Magiligimba.

 

Amewataja waliofariki dunia katika ajali hiyo kuwa ni Ramadhan Silaji, Godfrey Gaspar, Anthony Pastory, Mallya Wambura na Abdul Juma na kwamba miili ya marehemu imehifadhiwa katika chumba cha kuhifadhia maiti katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Shinyanga.

Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo,  baada ya ajali kutokea gari ndogo iliburuzwa na basi huku wakieleza kuwa dereva wa gari dogo alikuwa anaendesha kwa mwendokasi,

Toa comment