Ajali ya Basi, Lori na Trekta Yaua Kwimba, Mwanza
WATU ambao idadi yao bado haijafahamika wamefariki dunia na wengine kujeruhiwa baada ya basi la Frester, lori na trekta lilolokuwa limebeba mawe kugongana usiku wa kuamkia leo (Agosti 23, 2017) katika barabara ya Mwanza – Shinyanga eneo la Hungumalwa wilayani Kwimba.
Taarifa za awali zimeeleza kuwa, miili ya marehemu hao imehifadhiwa katika Hospitali ya Wilaya ya Ngudu huku majeruhi wakikimbizwa katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza kwa matibabu.
Taarifa hizo pia zimeeleza kuwa dereva wa basi hilo alikuwa amenasa ndani ya basi lakini hakupoteza maisha.
Usipitwe na Matukio, Install ===>Global Publishers App