Ajali ya Basi na Lori la Mizigo Yaua Watu 19, Nakuru

NAKURU, KENYA: Watu 19 wamepoteza maisha na wengine kadhaa wamejeruhiwa baada ya basi kugongana uso kwa uso na lori nchini Kenya.

Ajali hiyo imetokea eneo la Mbaruk Jumamosi katika barabara kuu ya Nakuru-Nairobi, Mkuu wa polisi Nakuru, Hassan Barua amesema.

Basi hilo ambalo ni mali ya kampuni ya Highway Sacco lilikuwa linaelekea Busia likitokea Nairobi wakati ajali hiyo inatokea.

Kamanda Barua amesema dereva wa basi hilo alikuwa anajaribu kulipita lori ndipo alipogonga gari la mzigo lilokuwa linakuja mbele yake.

Dereva huyo alikimbia baada ya kutokea ajali hiyo, wamesema polisi.

Watu kumi na nne wamelazwa hospitali ya St Mary Nakuru, Shadrack Musau ambaye ni muuguzi wa zamu amesema.

Hali Ilivyo Sasa kwa Wanafunzi Walionusurika na Ajali Arusha


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment