Ajali ya Lori na Basi Mwandege Mkuranga Yajeruhi

Lori la Mchanga lililokuwa likielekea Mkuranga limegongana uso kwa uso na daladala linalofanya safari zake Temeke kuelekea Kisemvule katika kijiji cha Mwandege Mkuranga mkoani Pwani.

Kwa taarifa za awali zinaeleza kuwa chanzo cha ajali ni dereva wa daladala aliyekuwa akijaribu kulipita Lori hilo la mchanga ndipo akaangukia pembezoni mwa msitu wa hifadhi ya Vikundu, ambapo inadaiwa kuwa dereva wa lori aliyejulikana kwa jina moja la Kinje hali yake si nzuri na amekimbizwa hospitali.

 

Kwa mujibu wa mashuhuda katika eneo hilo wamesema kuwa abiria waliokuwa kwenye daladala wameumia na kukimbizwa hospitali ya Mbagala rangi tatu, hata hivyo tunaendelea kumtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Pwani kuthibitisha hili.

Toa comment