The House of Favourite Newspapers

Ajali ya Ndege Yaua Watu 30 Pakistan

0

Ndege ya Shirika la Kimataifa la Ndege la Pakistani (Pakistan International Airlines) imeanguka katika Mji wa Karachi ilipokua ikitoka Lahore, maafisa wa safari za anga wamesema.

 

Ndege hiyo yenye namba PK8303, ambayo ilikua imewabeba watu 107 (abiria 91 na wahudumu wa ndege 8), ilikua ikisafiri kutoka Lahore kuelekea katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Jinnah wenye shuguli nyingi zaidi nchini Pakistan.

 

Waziri wa Afya wa Jimbo amethibitisha vifo vya watu 30, lakini inahofiwa kuwa idadi ya vifo itaongezeka na kuwa ya juu zaidi. Picha zimekua zikionyeshwa eneo hali ya mbaya eneo la tukio katika makazi ya watu ya Model Colony.

 

 

Ndege hiyo aina ya Airbus A320, ilikua ikikaribia kutua wakati ilipoanguka karibu na eneo la Model Colony, lililopo mjini Karachi yapata kilomita 3.2 (maili mbili) Kaskazini- mashariki mwa mwa uwanja wa ndege wa kimataifa wa Jinnah. Msemaji wa Shirika la Ndege la Pakistan amesema kuwa ndege hiyo ilipoteza mawasiliano na kitengo cha uongozaji wa ndege baada ya saa nane unusu mchana kwa saa za Pakistan.

 

 

Jeshi la Pakistan limesema kuwa limeweza kufika eneo la ajali haraka kupitia kikosi chake cha dharura na kusaidia juhudi za uokozi. Picha za Televisheni zinaonyesha wafanyakazi wa uokozi wakitengenisha vifusi vya ndege vilivyotapakaa kwenye mitaa ya makazi ya Model Colony, ambako nyumba kashaa zimeharibiwa kufuatia ajali hiyo.

Waziri mkuu wa jimbo la Sindh ambako ndege hiyo imeanguka, ametangaza hali ya dharura katika hospitali zote za Karachi.

Sababu ya ajali hiyo bado haijafahamika. Naibu Mkuu wa kampuni ya ndege ya kimataifa ya Pakistan- Arshad Malik amesema kuwa rubani alikua amekiambia kituo cha uongozaji wa ndege kwamba ndege ina “matatizo ya kiufundi”.

Waziri Mkuu wa Pakistan, Imran Khan amesema ”ameshitushwa na kuhuzunishwa” na ajali na akaahidi uchunguzi utafanyika mara moja kubaini chanzo cha ajali hiyo.

 

Ajali hii imetokea siku chache tu baada ya nchi hiyo kuanza kuruhusu ndege za kibiashara kufufua safari zake baada ya amri ya kutotoka nje katika kipindi hiki cha janga la corona.

 

Raia wa Pakistan kote nchini wanajiandaa kusherehekea sherehe ya Idd inayokamilisha mwezi wa Ramadhani, huku wengi wakisafiri kurudi makwao katika miji na vijijini.

Je hali ya usalama wa ndege wa Pakistan ikoje?

Pakistan inarekodi ya hali isiyo ya kusuasua ya usalama wa ndege, ikiwemo ajali kadhaa za ndege zinazoanguka.

 

Mnamo mwaka 2010, ndege iliyokua ikimilikiwa na kampuni ya binafsi ya ndege ya Airblue ailinguka karibu na Islamabad, na kuwauwa wasafiri wote 152 waliokuwemo ndani – ambao ulikua ndio mkasa mbaya zaidi ya ndege kuwahi kushuhudiwa katika historia ya Pakistan.

Mnamo mwaka 2012, Boeing 737-200 iliyokua ikimilikiwa na kampuni ya Pakistan- Bhoja Air ilianguka ilipokua ikitua katika mji wa Rawalpindi, na kuwauwa watu abiria wote 121na wahudumu sita.

Na mwaka 2016, ndege ya kampuni ya kimataifa ya ndege ya Pakistani -Pakistan International Airlines, iliungua ilipokua ikisafiri kutoka Kaskazini mwa Pakistan ikielekea Islamabad, na kuwauwa watu 47.

Leave A Reply