
Ajali ya Treni ya Abiria Yatokea Mkoani Tabora, Mabehewa Yaanguka
Ajali ya Treni mkoani Tabora
MABEHEWA sita ya treni ya abiria iliyokuwa ikitoka Mkoa wa Kigoma kuelekea Mkoani Tabora mpaka Dar es salaam yameanguka katika eneo la Kata ya Malolo iliyopo katika manispaa ya Tabora
Treni ikiwa imepata ajali eneo la Malolo mkoani Tabora
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Tabora, ACP Richard Abwao amesema kuhusu majeruhi na vifo bado jeshi linaendelea kufuatilia kutokana na abiria wengi kukimbizwa katika hospitali ya Mkoa wa Tabora Kitete kwa ajili ya matibabu.
Aidha, Kamanda Abwao amesema chanzo cha ajili hiyo mpaka Sasa bado hakijulikani na ufuatiliaji bado unaendelea.

