The House of Favourite Newspapers

Ajali Ya Treni Ya Mizigo Usiku Huu Moro, Ilikuwa Na Mabehewa 5, Treni Masta Afunguka – Video


Treni ya mizigo kwenye Reli ya kati iliyokuwa inatokea Dar es Salama kuelekea Isaka imepata ajali katika eneo la Bigwa Manispaa ya Morogoro.

Stesheni Masta Msaidizi Morogoro Bw. Godfrey Temba amesema Treni hiyo ambayo ilikuwa imebeba mzigo wa ngano, ilikuwa na Mabehewa 20 ambapo kati ya hayo, Mabehewa matano yamepinduka .

Temba amesema bado chanzo cha ajali hiyo hakijafahamika kwa sasa mafundi wanaendelea na uchunguzi kubaini chanzo chake lakini hakuna madhara kwa binadamu.