The House of Favourite Newspapers

Ajali Ya Treni Yasababisha Maandamano Makuba

Maandamano makubwa yanaendelea nchini Ugiriki huku serikali ikikabiliwa na shinikizo la kura ya kutokuwa na imani kufuatia ajali mbaya ya treni ya mwaka 2023.

Ikiwa ni kumbukizi ya miaka miwili tangu kutokea kwa ajali hiyo, waandamanaji wamesimamisha shughuli zote za kiuchumi wakitaka uwajibikaji wa kisiasa.

Mamia ya maelfu ya watu walimiminika mitaani Ijumaa kuadhimisha kumbukumbu ya pili ya ajali mbaya zaidi ya reli nchini humo, wakidai haki kwa waathiriwa.

Watu 57, wengi wao wakiwa wanafunzi, walifariki dunia katika ajali hiyo.