The House of Favourite Newspapers

Ajali Ya Treni Yaua 20

 

WATU 20 wamekufa na wengine 40 kujeruhiwa jijini Cairo, Misri, baada ya kutokea ajali ya treni katika njia kuu ya treni nchini humo. Tukio hilo limetokea baada ya treni hiyo kugonga kizuizi cha kupunguza kasi katika kituo kimoja cha treni katikati ya mji.

 

Ajali hiyo imesababishwa na kulipuka kwa tanki la mafuta la treni hiyo, hali iliyosababisha majengo ya jirani pia kuungua.

 

chanzo cha ajali hiyo bado hakijajulikana, lakini saa chache baadaye, Waziri anayeshughulika na usafiri, Hisham Arafat, alijiuzulu.

 

 

Watu walioshuhudia ajali hiyo wamesema wameona miili kadhaa katika janga baya zaidi kuikumba nchi hiyo katika siku za hivi karibuni, hususan kwa usafiri wa treni.

 

Mmoja wa mashuhuda, Ahmed Mahmoud, ameliambia shirika la Habari la AFP, kuwa alitoa miili ya watu 20 na kuiweka kwenye gari la wagonjwa, yote ikiwa imeungua vibaya.  Aidha amesema kwamba kwa kawaida treni likikaribia kituoni huja kwa mwendo wa taratibu, lakini siku hiyo lilikuwa katika mwendo kasi.

 

Awali vyombo vya habari vya nchi hiyo viliripoti kwamba watu waliofariki ni 25 huku wengine 50 wakiwa wamejeruhiwa. Waziri mkuu wa nchi hiyo, Mostafa Madbouli, ameapa kutoa adhabu kali kwa yeyote yule aliyehusika kupanga ajali hiyo.

 

Vilevile, Rais wa Misri, Abdul Fattah al Sisi,  ametuma salamu za rambirambi kwa familia za marehemu na kusisitiza kuwa watu wote waliojeruhiwa watapata msaada wowote watakaohitaji.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Comments are closed.