Kartra

Ajenga Nyumba ya Matairi, Inazunguka Ili Aone Jua, Wapita Njia

MZEE wa miaka 72 mkazi wa Srbac, nchini Bosnia anayejulikana kama Vokin Kusic ametumia zaidi ya miaka sita kukamilisha ujenzi wa nyumba ya kipekee yenye matairi inayozunguka baada ya kuchoshwa na malalamiko ya mkewe.

 

Kusic ameeleza kuwa aliamua kufanya hivyo baada ya mke wake kuzidisha malalamiko ambapo inadaiwa kuwa alikuwa anahitaji nyumba yenye muonekano tofauti zaidi ili awe na uwezo wa kuona kuchomoza kwa jua wakati huo huo na wapita njia katika eneo hilo.

Nyumba inaweza kuzunguka na kukamilisha mzunguko wa duara kwa saa 24 kama speed yake ni ndogo (slowest speed), lakini ikizungushwa kwa speed zaidi inaweza kutumia sekunde 22 pekee.

 

Kusic amesema kuwa magurudumu hayo yanamsaidia kuizungusha nyumba yake hali inayomfanya mkewe kupata nafasi ya kuona vitu vingine ambavyo havioni kutokana na kuzibwa na kuta za nyumba yake.

“Nimechoka na malalamiko yake na ukarabati wa mara kwa mara wa nyumba ya familia yetu na nikasema ningemjengea nyumba inayozunguka ili aweze kuizungusha na kuona vitu jinsi anavyotaka.” Alisema bwana huyo.


Toa comment