The House of Favourite Newspapers

Ajib: Yanga haijazuia ubingwa wa Simba SC

0

Ibrahim-AjibStraika wa Simba, Ibrahim Ajib.

Ibrahim Mussa, Dar es Salaam
STRAIKA wa Simba, Ibrahim Ajib, amewapoza mashabiki wa timu yake kwa kuwaambia kipigo cha mabao 2-0 ilichopata kutoka kwa Yanga, hakijazuia ndoto zao za kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara msimu huu.

Jumamosi iliyopita kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, Yanga iliifunga Simba katika mchezo huo namba 153 wa ligi kuu, mabao yao yakifungwa na Donald Ngoma na Amissi Tambwe.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Ajib alisema haoni sababu ya mashabiki wao kukata tamaa baada ya kufungwa na Yanga kwani Simba ina kikosi imara cha kuwania ubingwa msimu huu.
“Hakuna anayefurahia kufungwa, lakini kwa sababu imeshatokea haina jinsi zaidi ya kujipanga kwa ajili ya michezo inayofuata ili tujue ni namna gani tunaweza kutimiza lengo letu la kuwa mabingwa.
“Mashabiki watulie kwani nafasi ya ubingwa bado tunayo na hakuna timu ambayo imeweza kujihakikishia ubingwa hadi sasa kutokana na upinzani uliopo, mashabiki watuunge mkono,” alisema Ajib.
Simba kesho Jumapili kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, itacheza na Singida United katika mchezo wa kuwania kucheza robo fainali katika Kombe la FA.

Leave A Reply