Ajibu ajipanga kuimaliza Azam FC

NAHODHA wa Yanga, Ibrahim Ajibu amesema wamejipanga vizuri kuona wanapata matokeo baada ya kupoteza mchezo uliopita ingawa ni mchezo ambao anaamini utakuwa na ushindani.

 

Yanga katika mchezo uliopita uliopigwa Morogoro dhidi ya Mtibwa Sugar walipoteza kwa bao 1-0 na kusalia na alama zao 74 baada ya michezo 32.

 

Timu hiyo Aprili 29, mwaka huu, itavaana na Azam FC kwa mara ya kwanza msimu huu kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.

 

Akizungumza na Championi Ijumaa, Ajibu alisema: “Sisi Yanga tumejipanga vyema kupambana kuona tunapata matokeo mbele ya Azam FC ila hautakuwa mchezo rahisi kama wengi wanatarajia kila timu imetoka kuumia na inahitaji kupata matokeo.

 

“Kwa sasa tunaendelea na maandalizi kwa jumla na kuona tunarekebisha mapungufu yote ambayo tulifanya kwenye mchezo uliopita, mechi hii ya Azam kwetu ni muhimu.” Msimu huu Ajibu alianza vizuri lakini hapo katikati alipotea ambapo mpaka sasa amefunga mabao sita na kutoa asisti 15.

Loading...

Toa comment