Ajibu arejea Yanga, aahidi ushindi

LICHA ya kwamba Wanayanga wengi wameanza kuwa na wasiwasi nae, lakini Ibrahim Ajibu amerejea kikosini na mechi ijayo na Mtibwa atacheza.

 

Ajibu amekosa mechi tatu za Yanga mfululizo huku ikiripotiwa kuwa nyota huyo alikuwa akisumbuliwa na nyama za paja, ingawa Yanga wanaamini anakaribia kutua Msimbazi.

 

Nyota huyo amekosa mechi dhidi ya Lipuli FC, Ndanda FC, African Lyon na Kagera Sugar ambazo Yanga imecheza hivi karibuni katika Ligi Kuu Bara.

Akizungumza na Spoti Xtra, Ajibu alisema; “Kwa sasa ninaendelea vizuri na nimepona tofauti na awali ndiyo maana nilianza mazoezi mdogomdogo na sasa tayari nimeungana na timu kuendelea na mazoezi kama kawaida.”

 

“Hivyo nimerejea kuendelea kuipambania timu yangu, tutaendelea kupambana mpaka hatua ya mwisho na kuweza kufanya vyema,” alisema Ajibu.

 

Mpaka sasa katika mechi ambazo amecheza Ajibu msimu huu, ametoa asisti 15 na kuweza kufunga mabao sita na mkataba wake ndani ya Yanga unaenda kufika kikomo mwishoni mwa msimu huu na amekuwa akihusishwa na ishu ya kutaka kurejea Simba.

 

Kocha mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera amefunguka kuwa vijana wake wapo fiti kuvaana na Mtibwa Sugar na tayari siku ya kesho Jumatatu, watatua mjini Morogoro kwa maandalizi ya mchezo huo.


Loading...

Toa comment