Ajibu ataja vigezo vya nahodha Yanga

Ibrahim Ajibu enzi akiwa Yanga.

MSHAMBULIAJI wa Simba, Ibrahim Ajibu, amesema kuwa kigezo namba moja ambacho Yanga wanatakiwa kutumia ili kumteua nahodha mpya, ni kutazama yule anayeweza kuongoza.

 

Ajibu alijiunga na Simba hivi karibuni akitokea Yanga ambapo alikuwa nahodha wa timu hiyo na sasa inatakiwa kutafuta nahodha mwingine.

 

Akizungumza na Championi Jumatano, Ajibu alisema kuwa nahodha ni kiongozi ndani ya uwanja, hivyo anayestahili kutwaa kitambaa hicho kwa Yanga ni yule mwenye uwezo wa kuongoza.

 

“Ninaamini suala la nahodha wa timu hilo halipo mikononi mwangu zaidi ya Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera mwenyewe kuamua nani anastahili kuvaa kitambaa cha unahodha na anayestahili ni yule mwenye uwezo wa kuongoza.

 

“Yanga ina wachezaji wengi wazuri na wanajua kutimiza majukumu yao ndio maana tulikuwa tunashirikiana ila kwa sasa sipo huko nimerejea Simba, kocha mwenyewe atajua kwa kutazama vigezo ambavyo ni pamoja na nidhamu,” alisema Ajibu.

VITUKO Vya RC MWANRI Stejini Wasafi Festival “SUKUMA NDANI”


Loading...

Toa comment