The House of Favourite Newspapers

Ajibu Azua Hofu Yanga, Lwandamina Apagawa

0

WAKATI uongozi wa Yanga hivi sasa ukiwa katika harakati zake za kuhakikisha unakiimarisha kikosi chake ili kiweze kufanya vizuri katika mechi zake za Ligi Kuu Bara msimu huu zilizobakia, mshambuliaji wa timu hiyo, Ibrahim Ajibu amezua hofu kubwa klabuni hapo.

 

Uongozi wa timu hiyo umeingiwa na hofu kubwa baada ya kupokea taarifa kutoka kwa meneja wa timu hiyo, Hafidhi Saleh kuwa Ajibu hatakuwepo katika kikosi cha timu hiyo kitakachocheza dhidi ya Mbao FC.

 

Ajibu ataukosa mchezo huo kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kutokana na kuwa na kadi tatu za njano.

 

Ajibu ambaye pia mpaka sasa ameshazifumania nyavu mara tano, kadi yake ya kwanza aliipata katika mechi dhidi ya Kagera Sugar kwenye Uwanja wa Kaitaba mjini Bukoba, kadi ya pili ni katika mchezo dhidi ya Simba na ya tatu ni dhidi ya Prisons.

 

Akizungumza na Championi Jumatatu, Meneja wa Yanga, Hafidhi Saleh, alisema: “Benchi letu la ufundi linaangalia ni mchezaji gani atakayeziba nafasi yake katika mechi hiyo ambayo tutacheza mara tu baada ya kumalizika kwa michuano ya Chalenji.”

Sweetbert Lukonge, Dar es Salaam.

Leave A Reply