Ajibu, Manula Mambo Safi Simba

Kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu.

WACHEZAJI wa Simba, mlinda mlango, Aishi Manula na kiungo mshambuliaji, Ibrahim Ajibu wanajiunga na kikosi hicho baada ya kutoka kwenye majeraha huku mshambuliaji Wilker da Silva hali yake ikiwa bado haipo sawa. Manula alipatwa na majeraha katika mashindano ya Afcon, Ajibu na Da Silva wakiwa wanasumbuliwa na magoti.

 

Akizungumza na championi Jumatano, Daktari wa Simba, Yassin Gembe amesema kuwa, Ajibu na Manula wapo katika hatua za mwisho ya matibabu hivyo watarudi ndani ya wiki hii.

 

“Wachezaji wote wa Simba wapo fiti isipokuwa wale watatu tu ambao walikuwa majeruhi tangu awali.

“Ajibu na Manula wapo katika matibabu ya mwisho na ndani ya siku mbili hizi wanaweza kujiunga na wenzao kuendelea na mazoezi kwa kuwa wapo katika hatua nzuri.

 

“Isipokuwa Da Silva ndiyo bado goti linaendelea kumsumbua, yeye anaendelea na matibabu na haijajulikana lini atakuwa fiti, lakini kuhusu kina Manula kucheza mchezo wa marudiano na UD do Songo inategemea na watakavyokuwa fiti, mwalimu ndiye atakayeamua,” alisema Gembe.

UCHAMBUZI: HALI Za MAJERUHI Wa AJALI Ya MOTO | GLOBAL RADIO


Loading...

Toa comment