The House of Favourite Newspapers

Ajibu, Mkude Wafungiwa Vioo Simba

0

Khadija Mngwai | CHAMPIONI JUMATATU| Dar es Salaam

UONGOZI wa Klabu ya Simba umeonekana kuwafungia vioo wachezaji wake wawili mshambuliaji Ibrahim Ajibu na kiungo Jonas Mkude kwa kutofanya nao mazungumzo yoyote hadi sasa licha ya kuwa mbioni kumaliza mikataba mwishoni mwa msimu, kwa kuwa mtazamo wao kwa sasa ni ubingwa tu.

Ajibu na Mkude ni miongoni mwa wachezaji wanaotegemewa na Simba katika kikosi cha kwanza huku wakitarajia kumaliza mikataba yao mwishoni mwa msimu huu ambapo awali walionekana kugomea mazungumzo.

Akizungumza na Championi Jumatatu, bosi kutoka Simba ambaye hakutaka kutaja jina lake, alisema kwa sasa viongozi wamesimamisha kila kitu ikiwa ni pamoja na mazungumzo na wachezaji wanaotarajia kumaliza mikataba yao hivi karibuni na badala yake wanaangalia ubingwa ambao hawajaupata kwa misimu kadhaa sasa.

“Kila mtu kwa sasa hayupo sawa anachokiangalia ni kuona timu inafanikiwa kutwaa ubingwa wa ligi msimu huu, hivyo kuna mambo mengi ambayo hayaendi kwa sasa na badala yake watu wanaangalia jinsi ya kupambana ili kuweza kutwaa ubingwa.

“Hakuna hata kiongozi mmoja anayefanya mazungumzo na Ajibu wala Mkude wala mchezaji yeyote na wala sijasikia kuzungumzia suala hilo, viongozi wote wamekuwa wakihamasisha timu ijitume kwa kupata matokeo mazuri na kufanikiwa kutwaa ubingwa na ikimalizika ligi ndio mitazamo itakapohamia kwenye usajili,” alisema bosi huyo.

Championi Jumatatu lilipomtafuta Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili wa Simba, Zacharia Hans Poppe alisema kwa sasa hawaangalii masuala ya usajili hadi ligi itakapomalizika.

Leave A Reply