Ajibu Yamkuta Simba, Pablo Amuondoa Kikosini

KOCHA Mkuu wa Simba, Mhispania, Pablo Franco, amemuondoa kiungo mshambuliaji wa timu hiyo,
Ibrahim Ajibu katika mipango yake.

Hiyo ni katika kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting ambao utapigwa leo Ijumaa saa 10:00 jioni kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


Pablo, huo utakuwa mchezo wake wa
kwanza wa mashindano kukaa kwenye benchi akiiongoza timu hiyo akisaidiana na wasaidizi wake, Thiery Hitimana na Selemani Matola.


Mwenyekiti wa timu hiyo, Murtaza
Mangungu ameliambia Championi Ijumaa kuwa kiungo huyo atakosekana katika mchezo huo baada ya kupata majeraha katika mazoezi ya mwisho ya timu hiyo.

 

Mangungu alisema kuwa kiungo huyo alijikwaa uwanjani akifanya mazoezi kwenye Uwanja wa Boko Beach Veterani jijini Dar es Salaam.


“Ajibu hatakuwepo katika sehemu ya kikosi
kitakachocheza dhidi ya Ruvu kesho (leo) kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


“Ni baada ya kupata majeraha mazoezini,
alijikwaa mguuni akiwa anakimbia na kusababisha kupata maumivu,” alisema Mangungu.

STORI: WILBERT MOLANDI NA MUSA MATEJA

FULL VIDEO: HARMONIZE KAFUNGUKA YOTE KUHUSU DIAMOND, AVUJISHA SAUTI YA RAYVANNY – “WALISEMA NAROGA”3473
SWALI LA LEO

Kupanda Kwa Bei ya Mafuta Nchini, Nini Kifanyike Kupunguza Bei?
Toa comment