#GlobalCelebrityUpdates: Kiki Ama Nini? AKA na Bonang Matheba Watangaza Kurudiana!
Siku tatu baada ya kutangaza kuachana na mpenzi wake, rapa kutoka South Africa AKA na Bonang Matheba warudiana.
AKA na Bonang Matheba ni miongoni ya majina yanayobamba mitandaoni kwa pande za South Africa. Siku tatu baada ya Rapa AKA kuweka wazi kuwa amefika mwsiho wa reli na hawezi tena endelea kutumikia penzi lake kwa mrembo na mtangazaji Bonang Matheba, staa huyo wa HipHop anaonekana kufuta kauli hiyo kwa vitendo.
AKA ameamua kutetea penzi lake kwa Bonang Matheba kwa kumzawadia surprise ya pochi aina ya Gucci na kuomba pochi hiyo ipelekwe moja kwa moja ofisini kwa mrembo huyo, ikiwa kama ni ishara ya kumuomba msamaha kwa alichokitenda.
Kupitia Instagram account yake, Bonang Matheba alipost picha ya pochi hiyo na kuweka caption ya maneno isemayo:
“My heart can’t actually take it…!! Thank you baby…. Love! Love! Obsessed!! Dying… Surprises at work even?!I’m so spoilt… Thank you.”
Wapo wanaohisi kuwa hizi zote zilikuwa ni kiki tu za ku-promote wimbo mpya wa AKA ‘Ciaphus Song’ uliyoachiwa masaa machache yaliyopita. Je, wewe unaonaje? Niachie comment yako hapa chini.
Subscribe kwenye YouTube channel yetu Global TV Online ili uweze kupata updates zote za mastaa na burudani popote pale ulipo. Pia usiache kukaa karibu na sisi kupitia Instagram yetu @globalpublishers.
Comments are closed.