The House of Favourite Newspapers

Akamatwa Baada ya Kujificha Pangoni kwa Miaka 17

Polisi nchini China wamemkamata mhalifu ambaye amekuwa akijificha kwa miaka 17, baada ya kutumia ndege zisizokuwa na rubani kubaini pango alimokuwa akijificha.

 

Song Jiang (63) amekuwa akitafutwa na polisi baada ya kutoroka jela ambapo alifungwa kwa kufanya biashara haramu ya kuwasafirisha wanawake na watoto, lakini aliweza kutoroka kutoka kwenye kambi ya jela mwaka 2002.

Amekuwa akiishi ndani ya pango dogo na kukata mawasiliano ya aina yoyote na binadamu kwa miaka mingi. Polisi katika mji wa Yongshan walipokea taarifa kuhusu ni wapi alipo Song mwezi Septemba , kulingana na maelezo yao katika akaunti yao ya mtandao wa kijamii wa WeChat.

 

Taarifa hizo ziliwapeleka hadi katika eneo la milima iliyopo nyuma ya mji anakotoka katika jimbo la Yunnan lililopo kusini mashariki mwa Uchina. Baada ya kushindwa kumpata katika msako wa kawaida , maafisa walituma ndege zisizokuwa na rubani za ziada ili kuwasaidia maafisa katika msako huo.

Hatimae ndege hizo zilibaini chuma chenye rangi ya kwenye eneo la mtelemko mkali pamoja na taka zilizokuwa kando ya makazi yaliyopo karibu na eneo hilo. Ndipo polisi walipoamua kutembea kwa miguu hadi katika eneo hilo na kumpata song ndani ya pango dogo ambamo amekuwa akiishi kwa miaka.

 

Kwa mujibu wa polisi , mwanamme huyo amekuwa akiishi kwa kujificha binadamu kwa muda mrefu kiasi kwamba ilikuwa ni vigumu kwakekuwasiliana na maafisa usalama. Vyombo vya habari vya taifa vimesema kuwa Song alitumia chupa za plastiki kuteka maji kutoka mtoni, na matawi ya miti kama kuni za kuwasha moto. Baada ya kukamatwa amerudishwa tena gerezani.

Chanzo: BBC swahili

 

Comments are closed.