Akamatwa na maiti akisafirisha kwenye treni

 

MWANAMME mmoja anashikiliwa na vyombo vya dola baada ya kukutwa akisafiri na maiti ya mtoto kwenye treni ikiwa kwenye mfuko wa Malboro huko Malawi.

 

James Majawa mwenye umri wa miaka 28 alikuwa akisafiri kutoka Limbe kwenda Nayuchi. Maiti ya mtoto huyo ilibainika baada ya harufu ya kitu kilichoharibika kuenea kwenye treni hiyo.

 

Baada ya upekuzi ndipo maiti hiyo ikabainika huku ikiwa imetolewa sehemu za siri. Mtuhumiwa huyo alipohojiwa alieleza kuwa alikuwa anapeleka mwili huo kijiji cha Phalula huko Balaka.

 

Vyombo vya sheria vimesema  vinaendelea kumfanyia uchunguzi ili kugundua jambo hilo kiundani zaidi. Mtuhumiwa huyo amefunguliwa mashtaka ya kosa la jinai kwa kukamatwa na mwili wa binadamu.   Inaelezwa kwamba tukio hilo limekaririwa kuwa la imani za kishirikina.

 

JIUNGE NA FAMILIA YA GLOBAL TV UPANDE MTANDAO WA MAFANIKIO

Bofya hapa kujiunga na familia ya Global TV Club ==> Global TV Family Club

Loading...

Toa comment