Akamatwa na Silaha Zaidi ya 1,000

 

MWANAMME  mmoja nchini Marekani anashikiliwa na jeshi la polisi nchini humo kwa kukutwa na silaha mbalimbali za moto zikiwemo bunduki zaidi ya 1,000 katika makazi yake huko Los Angeles.

 

Ripoti za awali zilisema kwamba mtu huyo alikuwa haishi hapo palipokutwa silaha hizo bali anaiishi Ulaya,  lakini vyombo vya sheria vimethibitisha kwamba vimemtia nguvuni.

 

Kwa mujibu wa msemaji wa polisi mjini Los Angeles, mtuhumiwa alikuwa akifuatiliwa kwa kufanya biashara haramu ya silaha kinyume na utaratibu.

 

Hakuna madhara yoyote kwa umma na polisi kwa jumla yaliyopatikana kabla na baada ya kukamata silaha hizo za moto ambazo ni zaidi ya 1,000

 

Huyo anakuwa mtu wa pili kukamatwa na kiwango kikubwa cha silaha baada ya mwanamme mwingine kukutwa na silaha 1,200 zenye uzito wa tani 7, mwaka 2015.


Loading...

Toa comment