
JESHI la Polisi mkoani Mara wanamshikilia mwanamke mmoja aitwaye Nyangi Ismael kwa tuhuma za kumkata sehemu za siri mpenzi wake, Joseph Nyanakwi, wakiwa gesti baada ya kushindwa kumlipa Tsh. 5,000 walizoahidiana kulipana kwa kila mshindo mmoja wakati wa tendo la ndoa.
“Tulianza vinywaji tukakubaliana kila mshindo Tsh 5,000 akaomba kwanza Tsh 20,000 nikampa, tumelala kila nikimaliza mzunguko nikawa nalipa Tsh 5,000, kwa hiyo mizunguko mitatu nililipia Tsh 15,000, lakini huu wa nne nikamwambia kata kwenye ile Elfu 20 akagoma.
“Kumbe alikuwa na wembe ghafla alfajiri akashika uume wangu na kuanza kuukata kuanzia chini kwenye korodani nilipambana lakini akawa ameshaniumiza vibaya,” alisimulia Nyanakwi na kuongeza kwamba alipiga kelele watu wakajitokeza kumsaidia na kutoa taarifa polisi waliofika na kuwachukua wote na mwanamke huyo maarufu kama Mnyamongo ambaye polisi wamekiri kumshikilia.

