The House of Favourite Newspapers

Akifanya Hivi, Blac Chyna Atamfikisha Ferrari Mahakamani

0

Labda ulikuwa ukilisikia lile vuguvugu la ugomvi mkubwa baina ya watu waliowahi kuwa wapenzi, Blac Chyna na mwanamuziki Ferrari. Ishu ni kwamba katika kipindi ambacho Chyna akiwa na Rob Kardashian, kumbe kisirisiri alikuwa akibanjuka na Ferrari kitu kilichomfanya mwanamuziki huyo kumpiga picha za utupu mwanamke huyo kisha kuachia picha moja tu huku akisema kwamba nyingine ambazo zitamuonyesha mwili mzima zitafuata.

Post aliyoiweka Ferrari ya picha hiyo.

Hali hiyo imemchanganya sana Chyna kiasi cha kuongea na mwanasheria wake, Lisa Bloom na kutoa uamuzi kwamba kama mwanaume huyo ataendelea kuweka picha za namna hiyo walizopiga chumbani basi atamfikisha mahakamani haraka iwezekanavyo.

Je, Ferrari atatulia baada ya mkwara huo au atajifanya kutokujali? Yetu macho.

Na: Nyemo Chilongani, GPL

 

LIVE: Kuaga Mwili wa Marehemu ‘Bikira wa Kisukuma’, Leaders Club

Leave A Reply