The House of Favourite Newspapers

Akili za Fei Toto Zinawaza Kufunga

0

KIUNGO wa Yanga, Feisal Salum, ‘Fei Toto’ amesema kuwa akiwa uwanjani yeye anawaza kufunga ama kutengeneza nafasi ya bao kwa ajili ya timu yake ili iweze kupata ushindi.

Mzawa huyo kibindoni ana mabao mawili ambapo alikuwa wa kwanza kufunga ndani ya Yanga na aliwatungua Kagera Sugar, Uwanja wa Kaitaba na bao la pili aliwatungua KMC, Uwanja wa Majimaji, Songea.

Akizungumza na Championi Jumatatu, Fei Toto alisema kuwa hakuna jambo ambalo huwa anawaza akiwa uwanjani zaidi ya kufunga kwa kuwa ni kazi yake.

“Kazi yangu mimi ni mpira na nikiwa uwanjani huwa ninafikiria kufunga ama kutengeneza nafasi ya kufunga kwa mwenzangu kwani kila tunapoingia uwanjani tunahitaji ushindi.

“Sipati tabu kwenye kufunga kwa kuwa kwenye kila mazingira huwa ninakuwa ninajua hapa ninapaswa nipige mpira kwa mtindo gani inakuwa rahisi kwa sababu ni vitu ambavyo ninavifanyia mazoezi mara kwa mara,” alisema Fei Toto.

Kituo kinachofuata kwa Yanga yenye pointi tisa baada ya kumalizana na KMC ni Oktoba 30 itakuwa mbele ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa.

LUNYAMADZO MLYUKA, Dar es Salaam

Leave A Reply