Akilimali: Nimechangiwa Sh 1900

MWANACHAMA na Mjumbe wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali ameweka wazi kuwa juzi Alhamisi hii alipokea mchango wa Sh 1900 kutoka kwa wadau mbalimbali.

 

Fedha hizo zimetoka kwa baadhi ya wadau ambao wameguswa naye zikiwa ni kwa ajili ya kumsaidia kulipa deni la Sh 369,000 analodaiwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili baada ya kutibiwa kutokana na kusumbuliwa na Ugonjwa wa Kisukari.

 

Akizugumza na Championi Jumamosi, Akilimali alisema kiasi hicho alichangiwa kwa Alhamisi pekee lakini tangu Jumapili iliyopita ambayo ndiyo alianza kuchangiwa mpaka jana jumla alikuwa amekusanya Sh Sh 34,700 pekee.

 

“Alhamisi hii wamenitumia Sh 1,900, ndizo fedha nilizopokea, lakini tangu waanze kunichangia nimefikisha shilingi 34,700.

 

“Nawaomba wadau, haswa wanachama na mashabiki wa Yanga wazidi kunisaidia kwa chochote walichonacho ili niweze kulipa deni hili, maana nisipolipa mapema, huduma ambazo naendelea kupewa Muhimbili nitasitishiwa,” alisema Akilimali.

George Mganga, TUDARCo


Loading...

Toa comment