The House of Favourite Newspapers

Akimalizana na Yanga tu, Kocha Simba anaondoka

0

kazimoto na benchi la ufundi, simba

TIMU ifungwe, isifungwe hata ikitoa sare dhidi ya Yanga, Jumamosi ijayo katika Ligi Kuu Bara, Kocha wa viungo wa Simba, Dusan Momcilovic ni lazima aondoke nchini kurudi kwao Serbia.

Momcilovic anaondoka Simba baada ya kukamilika kwa kazi yake ya kuwaweka fiti wachezaji wa timu hiyo katika suala zima la stamina na pumzi muda wote wawapo uwanjani.

Tayari kazi ya Momcilovic imeonekana kuzaa matunda ambapo Simba imecheza kwa kasi na stamina kubwa na kupata ushindi katika mechi mbili dhidi ya African Sports (bao 1-0) na ile ya pili dhidi ya Mgambo JKT mabao 2-0.

Rafiki wa karibu wa kocha huyo, amelihakikishia Championi Jumamosi kuwa, Momcilovic yupo kwenye harakati za mwisho za kuondoka nchini baada ya kumaliza kazi iliyomleta kwani mkataba wake umeisha na hatoongezewa mwingine.

Alipotafutwa mwenyewe Momcilovic kuzungumzia hali hiyo, alisema: “Nimeifanya kazi yangu kwa ufasaha kabisa ndani ya Simba naamini kila mmoja ameiona, sasa wachezaji wana stamina na wanaweza kupambana muda wote.

“Siwezi kusema mengi lakini napenda kuwashukuru wale wote waliokuwa wakinipa ushirikiano kwa kipindi hiki chote,” alisema Momcilovic.

Gazeti hili linaamini kuwa, kazi iliyokuwa ikifanywa na kocha huyo sasa inaweza kufanywa hata na Kocha Msaidizi, Suleiman Matola na Momcilovic anaondoka ili kupunguza gharama za uendeshaji wa timu.

JIUNGE NA MICHEZO KIGANJANI TUMA NENO SPORTS KWENDA NAMBA 15778CHAMPIONI

Leave A Reply