Akina Mama Sinza Watabasamu Kupitia Msaada wa Meridianbet Hospitali ya Palestina

Tabasamu na hisia za shukrani zilitawala katika Hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar es Salaam, baada ya Meridianbet kutoa msaada wa Mama Packs kwa akina mama wajawazito na waliojifungua hivi karibuni. Msaada huo ulihusisha mahitaji muhimu ya mama na mtoto ikiwemo nguo za watoto, nepi, wipes, sabuni pamoja na taulo za kike, yakilenga kupunguza changamoto wanazokutana nazo katika kipindi cha uzazi.
Hatua hiyo ni sehemu ya mkakati mpana wa Meridianbet wa kushiriki kikamilifu katika masuala ya kijamii, hasa yanayogusa afya na ustawi wa jamii. Kupitia programu zake za Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR), kampuni hiyo imeendelea kuwa karibu na makundi yenye uhitaji maalum, ikitambua kuwa maendeleo ya biashara hayawezi kutenganishwa na maendeleo ya jamii.

Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Akizungumza katika tukio hilo, Nancy Ingram, Afisa Mawasiliano wa Meridianbet alisema kampuni inaamini kuwa mafanikio ya kweli hupatikana pale yanapoguswa na maisha ya watu wa kawaida. Alieleza kuwa msaada huo wa mwisho wa mwaka umetolewa kwa lengo la kuwapa akina mama faraja na matumaini mapya wanapoelekea kuanza mwaka mpya, huku wakipokea changamoto za malezi kwa moyo wa matumaini.

Uongozi wa Hospitali ya Palestina nao haukusita kupongeza mchango huo, ukieleza kuwa msaada huo umefika wakati muafaka na utasaidia kwa kiasi kikubwa kuboresha hali ya akina mama walioko hospitalini. Mwakilishi wa hospitali hiyo alisema kuwa Meridianbet imeonesha mfano mzuri wa kampuni binafsi inayochanganya biashara na uwajibikaji wa kijamii kwa vitendo.
Kwa ujumla, tukio hilo limeendelea kuithibitisha Meridianbet kama mdau anayejali ustawi wa jamii. Kupitia misaada ya kijamii katika sekta za afya, elimu, michezo na ustawi wa makundi maalum, kampuni hiyo inaendelea kujenga uhusiano chanya na jamii, ikionesha kuwa mafanikio ya biashara yanaweza kwenda sambamba na kugusa maisha ya watu kwa njia yenye maana.

