Akina Masogange, huyu Mkongo siyo

MASOGANGE5Ojuku Abraham

UNA mshkaji anaitwa Mwami Radjabu, wadau wanamtaja kama kijana mwenye uraia wa nchi jirani ya Kongo (DRC), kwamba ni mfanyabiashara mwenye ukwasi wa kutosha. Kutokana na mkwanja wa kutosha alionao, ana ukaribu na akina dada wengi wa Kibongo, hasa hawa wenye majina katika tasnia ya filamu, wenyewe tukiwajua zaidi kama Bongo Muvi.

Leo utasikia akitajwa kama Mkongo wa Wolper au wa Masogange, kesho yake watasema ameporwa na Hamisa Mabeto, mara utasikia sasa anajirusha na Husna Maulid na ghafla watasema hivi sasa anatesa na Wema Sepetu.

Na hawa madada wote wanaotajwa, ni mastaa wetu wanaofanya vizuri katika filamu na uanamitindo. Wamecheza sinema nyingi na kwa hakika, wanao mashabiki wa kutosha kote nchini. Kuna msemo unaosema, katika msafara wa mamba na kenge wamo. Usitegemee kuwakuta mastaa wa fani fulani katika kijiwe cha peke yao.

Kilakiwanja, wanakuwepo wote, Bongo Fleva, filamu, dansi, mitindo, soka na aina nyingine zote za michezo na burudani. Kwa maana hiyo, wakati msichana mmoja anapokuwa katika ukumbi f’lani wa burudani na mtu wake, mastaa wenzake nao wanakuwepo maeneo hayo, wakifanya yao.

jaqHivyo inakuwa rahisi kwa mfano, mwanaume asiyejulikana anayetembea na staa, kuwafahamu mastaa wengine, kama ambavyo mastaa nao wanavyoweza kumjua ‘shemeji’ yao asiye maarufu. Hiyo inamaanisha kesho akiibuka katika ‘kiwanja’ kingine cha starehe, hata kama hakuwa na mtu wake wa jana, ataweza kukutana na shemeji zake na kuendelea na makamuzi kama kawa.

Ni hapo ndipo tabu inapotokea. Labda ni kinywaji, labda ni ofa za maisha mazuri, labda ni mapenzi, lakini kinachotokea kinakera kukisikia, kwamba mwishowa mchezo, akina dada hawa wanageukana na kujikuta wote wakiunga ‘cheni’ kwa mtu mmoja. Lakini kinachosikitisha zaidi ni kusutana kunakotokea baada ya mambo yao kufahamika.

Ooh huyu ananichukulia bwana’angu, ananifuatafuata au anikome na kadhalika. Hili siyo jambo linalopendeza kulisikia kutoka kwa watu ambao jamii inawachukulia kama kioo.

Katika zamam hizi, hivi kweli watu bado wanachukuliana mabwana? Licha ya magonjwa, lakini pia haifurahishi kuona watu tunaoamini kuwa mastaa wakipanga foleni kwa mtu, eti tu kwa sababu ana pesa.

Hii inaonesha huenda hawana njia nyingine ya kujipatia kipato zaidi ya kutegemea waleti za wanaume. Kama hivi ndivyo, niwashauri dada zangu kuachana na staili hiyo ya maisha, kwa sababu licha ya kujidhalilisha wao wenyewe, lakini pia inaleta picha mbaya kwa mashabiki na wadau wengine wanaoweza kuwazuia watoto wao kujiingiza katika fani za umaarufu, wakihofia na wao wataishi kwa kutegemea wanaume! Dada zangu kuweni makini na Mwami aliyeamua kuwadilisha kama nguo.


Loading...

Toa comment