Akitema Mate Sakafu Inachubuka, Ndani Miaka 3 – Video

ANNA Majaliwa, mkazi wa Tabata jijiji Dar es Salaam, ni mama wa watoto watatu ambaye yupo ndani tangu 2017 kutokana na kusumbuliwa na maradhi ambayo licha ya kuzunguka hospitali mbalimbali bado hajafahamu ni ugonjwa wa aina gani hasa anaugua.
Anna ana miezi zaidi ya sita hajapata haja kubwa, hawezi kutembea, ulimi hauhisi ladha ya chakula, akitema mate sakafu inachubuka, ukimchoma moto hapati maumivu, hapati usingizi.
Chanzo cha yote ni kuharibika kwa ujauzito, ambapo Anna anasema pia baba watoto wake amemkimbia baada ya kupata maradhi hayo,
Baada ya kupata habari hizi kupitia mitandao ya kijamii klabu ya soka ya Yanga imetoa msaada ya vitu mbalimbali kwa ushirikiano wa wadhamini wao, GSM.

