The House of Favourite Newspapers

Akiwa Leba, Kucha Zataka Kumletea Balaa Maimarta

Maimartha Jesse

MTANGAZAJI maarufu Bongo, Maimartha Jesse amesimulia jinsi kucha zilivyotaka kumletea balaa alipokwenda kujifungua leba ambapo amewapa somo mastaa wa kike wanao-penda kubandika kucha kuwa makini hasa kipindi cha ujauzito.

 

Akizu-ngumza na Risasi Jumamosi, Maimartha alisema mara baada ya kuingia leba ilibaki kidogo afukuzwe na daktari kwani kucha alizokuwa amebandika zilikuwa zinageuka kuwa kero na kujikuta akizitoa kwa meno licha ya kwamba alikuwa akipata mau-wmivu.

 

“Yaani sitasahau maana kidogo tu nifukuzwe leba kisa kucha za kubandika, niwape tu tahadhari wenzwangu kuwa makini na kucha hizo maana siyo nzuri kabisa,” alisema Maim-artha.

Stori: Gladness Mallya

 

Comments are closed.