#GlobalUpdates: Akon Amchagua Muafrika Huyu Kuwa Muongozaji Mkuu Wa Video Zote Za Konvict Music Africa – (Video)

Imagine unapata shavu la kufanya kazi na Akon na unaenda kuwa Muongozaji wa video sio moja wala mbili bali video zote zinazotengenezwa chini ya kampuni ya Konvict Music Worldwide! Hizi bahati zina wenyewe na imemdondokea Muafrika huyu.

Kufanya kazi na kuaminiwa na staa mkubwa wa muziki kutoka Marekani sio kitu kidogo, actually ni ndoto ya watu wengi sana na pale bahati hiyo inapokuangukia kupagawa ni sehemu ya kuonyesha furaha yako.

Nimetembelea mtandao wa Instagram na huko nimekutana na post ya boss wa Konvict Music Worldiwide Akon akimtangaza muongozaji wa video Patrick Elis kutoka Nigeria kuwa official Video Director wa video zote za Konvict Music Worldwide branch ya Africa.

Patrick Elis.

Kupitia Instagram page yake, Patrick Elis alipost video mbili akiwa na Akon na kuweka caption inayosema: Is official let take the game to another level @akon @gproduction ” 

A post shared by @patrickelis on

Patrick Elis amesomea mambo ya Cinematography nchini Marekani na tayari ameshafanya kazi na baadhi ya wasanii wakubwa wa Africa na Nigeria ikiwemo Tekno na wengine.

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

 

 

Loading...

Toa comment