#GlobalCelebrityUpdates: Akothee Afanya Matanuzi Zurich Na Gari Jipya Aina Ya ‘Porsche Cayenne’ – (Pichaz).

Kwenye Celebrity Updates za leo April 07 2017 ninayo hii ya Madam Boss wa 254 Akothee kutokea pande za Zurich.

Waswahili husema; ‘Pesa ni sabuni ya roho’. Ukiwa na pesa mambo yako mengi yanaedna poa hata matanuzi yako yanakuwa tofauti kidogo na mtu mwenye kipato cha kawaida na Akothee ni mfano hai wa huu mtazamo.

Kwenye pita pita yangu Instagram nimekutana na picha tatu za Akothee akiwa Zurich kwenye ziara yake ya kimuziki ambako baada ya kufanya show msanii huyo akaamua kufanya matanuzi na kujinunulia gari jipya aina ya Porsche Cayenne na kupost picha za gari hilo jipya kwenye page yake ya Instagram.

Kupitia Instagram yake, Akothee amepost picha za gari hiyo na kuziwekea caption inayosema: #MADAMBOSS #porscheglasses #porschecayenne#Gamechanger Zurich by day…”

Zicheki picha za gari mpya ya Akothee hapa chini:

 

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Pichaz: Instagram/ AkotheeKenya

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

 

Loading...

Toa comment