The House of Favourite Newspapers

#GlobalCelebrities: Akothee Awakingia Kifua Single Mamas, Awatolea Povu Wale Wanaojifanya Wajuaji Wa Kulea! – (Soma)

 

Kwenye zile posts na captions za mastaa zinazotrend Instagram, ongeza na hii ya #MadamBoss Akothee kutoka Kenya ambaye ujumbe wake kwa watu wanaowasimanga single mamas umezua mjadala mkubwa mtandaoni.

Hit maker wa single ya TuchezeAkothee ni mama wa watoto watano na licha ya kuwa staa huyo alishawahi kukiri kuwa hobby yake kubwa ni kuzaa na kulea watoto, msanii huyo hajasita pia kuweka wazi kuwa baby daddy wake wa kizungu hajihusishi kwa namna yoyote ile kwenye malezi ya mwanae kwani mzungu huyo yupo radhi atumie pesa yake kutembea dunia nzima kula bata lakini sio kulea:

Nina babdy dady wakizungu ambaye yupo radhi atumie pesa yake kutembea dunia nzima na kufanya starehe za ngono, lakini hajawahi hata siku moja kuwajibika kumtunza mwanae wa pekee toka azaliwe… 😂😂😂😂. ” – Aliandika Akothee kwenye Instagram page yake.

Sasa leo kwenye pitapita yangu Instagram nimekutana na post ya msanii huyo ambaye alikuwa na jambo la kuwaambia watu wanaowasimanga Single Mamas. Hiki ndio alichokisema:

Eti Single Mothers wanatakiwa kubaki tu nyumbani kisa tu wana watoto! Sasa tayari wapo single mnataka nani awatafutie chakula? Next time ukikutana na  single mother popote, tafadhali usiulize maswali ya kukwaza kama ‘umemwaacha watoto na nani?’, kwasababu hata kama angekuletea hao watoto, usingewaweza… emu mtuaache, fanya yako #Madamboss.  ” – Akothee ameandika.

Imeandikwa Na: Sandra Brown.

Subscribe kwenye YouTube Chanel yetu ya Global TV Online ili zote kali zinazotufikia iwe ni siasa, michezo, comedy, burudani, stori za mastaamuziki na nyingine kali zikufikie kwa wakati.

Comments are closed.