The House of Favourite Newspapers

Al Ahly Yaitungua El Merreikh 3-0 (Video)

0

 

MABINGWA Watetezi wa Ligi ya Mabingwa Barani Afrika Al Ahly, ambao wapo kundi moja na  Simba SC  wakiwa nyumbani  wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya El Merreikh usiku wa kuamkia leo.

 

Mechi hiyo iliyopigwa katika Uwanja Uwanja wa Taifa wa Cairo, mabao ya Al Ahly yalipachikwa na Mohamed Magdy dakika ya 57, Kahraba dakika ya 63 na Walter Bwalya dakika ya 71 na kuwafanya Waarabu hao sasa waongoze kundi A kwa tofauti ya mabao na Simba huku wote wakilingana pointi.

 

Mchezo unaofuata wa miamba hiyo ya Afrika ni dhidi ya Simba Februari 23, kwenye uwanja wa Mkapa Dar es salaam. 

 

 

Leave A Reply