The House of Favourite Newspapers

Al Qaeda Yashambulia Burkina Faso

0

Burkina Faso (8)Mabomu yakilipuka kwenye hoteli ya Splendid mjini Ouagadougou.

Ouagadougou, Burkina Faso

Takriban mateka 30 wameokolewa baada ya wapiganaji kushambulia hoteli moja katika Mji Mkuu wa Ouagadougou nchini Burkina Faso na kusababisha mauaji ya takriban watu 20 na wengine 15 kujeruhiwa mapema leo Jumamosi.

Burkina Faso (12)Jengo la Hoteli ya Splendid

Watu kadhaa waliofunika nyuso zao walivamia hoteli hiyo ya Splendid na kuwateka watu kadhaa baada ya bomu kulipuka nje ya hoteli hiyo, kulingana na taarifa kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo.

Burkina Faso (9)Waziri wa Mawasiliano wa Burkina Faso, Remis Danjinou alituma ujumbe katika mtandao wa tweeter akisema takriban watu 30 wameachiliwa huru na kwamba oparesheni ya kijeshi kukabiliana na wapiganaji hao imeanza.

Burkina Faso (7)Polisi wakipambana na wapiganaji.

Amesema kuwa waziri wa nguvu kazi Clement Sawadogo ni miongoni mwa waliookolewa.

Burkina Faso (6)Hali ilivyokuwa.

]Tayari takriban watu 30 wamepelekwa hosptalini wakiendelea kupata matibabu aliongezea.

Burkina Faso (13)Haijajulikana iwapo kuna mateka ambao bado wamesalia katika hoteli hiyo, lakini mashahidi wameripoti milio mikali ya risasi katika ghorofa za juu mapema asubuhi.

Burkina Faso (14)Vikosi maalum vya Ufaransa pamoja na wanajeshi wa Burkinabe walihusishwa katika kuwaokoa mateka hao katika hoteli hiyo inayotumiwa na Umoja wa Mataifa pamoja na raia wengine wa Magharibi, alisema bwana Dandinou

Burkina Faso (4)Amesema kuwa idadi ya watu waliopoteza maisha yao haijulikani.

Burkina Faso (3)Waliojeruhiwa.

Afisa mkuu wa Hospitali Robert Sangare aliwanukuu baadhi ya manusura wakisema takriban watu 20 walifariki katika shambulio la kwanza, kabla ya vikosi vya usalama kuanza makabiliano na wapiganaji hao.

Burkina Faso (15)Baadaye, Waziri wa Mambo ya ndani wa nchi hiyo, Simon Compaore alisema kuwa miili 10 imepatikana karibu na mgahawa mwengine wa Cappucino ambao pia ulishambuliwa na wapiganaji hao.

Burkina Faso (16)Kundi moja linalofuatilia mitandao ya wapiganaji wa Jihad limesema kuwa wapiganaji wa al-Qaeda katika eneo la Maghreb wamekiri kutekeleza shambulizi hilo.Burkina Faso (11)Raia wa Ufaransa Leila Alaoui, ni mmoja kati ya waliojeruhiwa.Burkina Faso (2)Burkina Faso (5)

Leave A Reply