The House of Favourite Newspapers

Al Shabaab waua 15 hotelini Mogadishu

0

nyumba

Hoteli iliyoshambuliwa na Kundi la Al Shabaab.

TAKRIBANI watu 15 wamepoteza maisha katika shambulio lililofanywa na wanamgambo wa Al Shabaab katika hoteli moja mjini Mogadishu nchini Somalia leo.

gari

Magari yaliyokuwa na mabomu yakishambulia hoteli hiyo.

Hoteli hiyo ambayo iko kwenye moja ya mitaa yenye shughuli nyingi mjini humo mara nyingi hutumiwa na wabunge na maofisa wa serikali.

Kundi la Al Shabaab limethibitisha kutekeleza shambulizi hilo lililofanywa kwa kutanguliza magari mawili yaliyokuwa na mabomu ili kushambulia hoteli hiyo.

Vikosi vya Muungano wa Afrika vinasema kuwa vimechukua udhibiti wa hoteli hiyo baada ya mapigano makali.

Ripoti zinasema kuwa mlipuko huo ulifuatiwa na ufyatulianaji mkubwa wa risasi.

Credit: BBC

Leave A Reply