The House of Favourite Newspapers

Al-Shababab wasambaratishwa tena!

0

Al shabaab (2)

SIFAEL PAUL na Mtandao:

ILIPOISHIA WIKI ILIYOPITA:

Mpenzi msomaji wiki iliyopita tuliona jinsi ambavyo kundi korofi la kigaidi la Al Shabaab lilivyovamia Bunge la Somalia ambapo watu takriban kumi waliuawa huku zaidi ya 30 wakijeruhiwa vibaya ikiwa ni pamoja na wanajeshi 14 wa Somalia na watano wa Jeshi la Afrika la kulinda amani.

SASA ENDELEA…

SERIKALI ya Somalia imekuwa ikipambana na Al-Shabaab kwa miaka kadhaa sasa kwa msaada wa Jeshi la Umoja wa Afrika. Wakati hali ikiwa tete Somalia, kuliibuka habari mbaya kuwa Al- Shabaab walisababisha vifo vya karibu watu 15 katika shambulio lao lingine walilolitekeleza katika eneo la Poromoko katika Mji wa Mpeketoni, Kaskazini mwa Kenya.

Kwa mujibu wa Waziri wa Mambo ya Ndani wa Kenya, Joseph Ole Lenku, washambuliaji hao waliharibu kituo cha mawasiliano cha Safaricom kabla ya kuanza mashambulizi kwa lengo la kuwazuia wakazi wa maeneo hayo kuwasiliana na watu wa nje na kutoa onyo.

Tukio hilo lilikuja baada ya shambulio lingine kwenye mji huo ambapo watu 48 waliuawa na wakazi waliokuwa na hasira waliripotiwa kukusanyika wakimtaka waziri huyo kueleza kilichotokea. Baada ya kuona hali inakuwa tete, ilibidi Marekani iingilie kati ambapo jeshi lake liliushambulia mtandao wa Al-Shabaab katika operesheni yake nchini humo.

Shambulio hilo la Marekani lilitajwa kumlenga kiongozi wa kundi hilo aliyedaiwa kuwa mafi choni. Kwa mujibu wa taarifa ya Wizara ya Ulinzi ya Marekani, Pentagon, shambulio hilo lilikuwa likimlenga kiongozi huyo aliyekuwa mafi choni. Msemaji wa Pentagon, John Kirb alikaririwa akisema kuwa Marekani ilikuwa ikifuatilia kwa ukaribu operesheni zake ili kupata matokeo zaidi pale taarifa itakapopatikana.

Hata hivyo, hakukuwa na taarifa zaidi. Afi sa mwandamizi wa usalama nchini Somalia alisema kuwa kulikuwa na ndege iliyokuwa ikiruka bila rubani ikimlenga Kiongozi wa Al- Shabaab, Ahmed Abdi Godane, muda mfupi baada ya kuondoka katika mkutano wa viongozi wa mtandao huo. Godane alifahamika kama kiongozi wa kidini wa kundi hilo lenye mfungamano na mtandao wa kigaidi wa Al-Qaeda.

Afi sa mmoja wa Somalia aliyezungumza bila kutaja jina kutokana na kutokuwa na mamlaka ya kufanya hivyo, alisema kuwa taarifa za uchunguzi zilionesha kuwa kiongozi huyo huenda alikuwa ameuawa.

Taarifa zilieleza kwamba, shambulio hilo lilifanyika katika msitu ulio karibu na Wilaya ya Sablale, kilometa 170, Kusini mwa Mogadishu, eneo ambalo Al-Shabaab lililitumia kutoa mafunzo kwa wapiganaji wake.

Gavana wa Lower Shabelle nchini Somalia, Abdiqadir Mohammed Nor, aliliambia Shirika la Habari la AP kwamba majeshi ya serikali na Umoja wa Afrika yalielekea katika Mji wa Sablale na kwamba walisikia mzizimo kama wa tetemeko la ardhi wakati ndege zilizokuwa zikiruka bila rubani zilipoishambulia Kambi ya Al- Shabaab.

Marekani imeendelea kufanya mashambulizi ya angani nchini Somalia katika miaka ya hivi karibuni. Shambulio lake la kombora lilidaiwa kumuua afi sa wa ngazi za juu wa masuala ya usalama wa Al-Shabaab. Pia lilifanikiwa kulisambaratisha gari lililokuwa limebeba wanachama wa kundi hilo na kusababisha kifo cha mtaalam wa juu kabisa wa vilipuzi wa mtandao huo.

Hatua hiyo ya Marekani ilikuja baada ya majeshi ya serikali ya Somalia kufanikiwa kulirejesha katika udhibiti wake gereza kubwa mjini Mogadishu ambalo lilishambuliwa na watu saba wenye silaha nzito.

Ilisemekana kuwa watu hao waliohisiwa kuwa Wanamgambo wa Al-Shabaab, walikuwa katika jaribio la kutaka kuwaachia huru wenzao wengine wenye itikadi kali waliokuwa wamefungwa.

Hata hivyo, taarifa ya Pentagon haikueleza kama shambulio hilo lilihusiana na lile la gereza au la. Baadhi ya maafi sa nchini Somalia walikaririwa wakisema kwamba, washambuliaji wote, wanajeshi watatu wa serikali na raia wawili waliuawa.

Gereza la Godka Jilacow la mjini Mogadishu ni kituo cha mahojiano cha idara ya upelelezi ya Somalia ambapo kunaelezwa kuwepo kwa wafungwa kutoka Al-Shabaab ambao walikuwa wakishikiliwa chini ya ardhi.

Je, nini kiliendelea? Usikose wiki ijayo.

Leave A Reply