The House of Favourite Newspapers

Ala kichapo, achimbiwa kaburi

0

kaburi (2)Kijana Juma Rajabu akionekana mwenye majeraha.

Na Haruni Sanchawa

Kijana mmoja aliyetambulika kwa jina la Juma Rajabu, 23, (pichani) mkazi wa Kijiwe Samli Wilaya ya IIala, Dar nusura auawe baada ya kula kichapo maeneo ya Buguruni Sheli, hali iliyofanya afikishwe na polisi Hospitali ya Amana jijini Dar es Salaam kwa matibabu.

kaburi (3)
Chanzo chetu kilisema kijana huyo alipigwa hadi kupoteza fahamu na wabaya wake waliodai kuwa aliwaibia na baada ya kichapo waliamini kuwa amefariki dunia.

“Vijana wale baada ya kumpiga naye kupoteza fahamu wakajua kuwa wamemuua, hivyo wakamuacha palepale hadi polisi wa doria walipofika na kumchukua,” kilisema chanzo ambacho hata hivyo haikuelezwa alituhumiwa kuiba nini.

kaburiHabari zinasema baadhi ya watu wanaomfahamu kijana huyo walifikisha habari nyumbani kwao wakidai kuwa ameuawa na maiti yake ipo Hospitali ya Amana, hivyo maandalizi ya mazishi yakafanyika.

“Jumamosi asubuhi familia yao baada ya kupata taarifa za ‘msiba’ waligawana majukumu, wapo waliokwenda kuchumba kaburi, wapo waliokwenda kununua sanda na upishi wa chakula ulifanyika,”alisema mama mzazi wa  kijana huyo aliyejitambulisha kwa jina la Tatu Mohamed  (65).

Bi Tatu alisema  kila aliyepewa  jukumu lake  lilifanya na  waliokwenda Hospitali ya Amana walipofika walimkuta Juma akiwa hai ila akiwa ameumizwa na kushonwa nyuzi kadhaa sehemu mbalimbali za mwili wake.

“Watu waliokwenda Amana walituarifu kwa simu kwamba Juma hajafariki dunia, hivyo shughuli za msiba zikasitishwa mara moja na watu wakatangaziwa na wakatawanyika.

Alipohojiwa na gazeti hili Juma alisema kuwa alipigwa na  na watu asiowajua baada ya kusingiziwa kuwa ni mwizi.

Leave A Reply