The House of Favourite Newspapers

ALAF Limited Yawapa Ufadhili Wanafunzi wa UDSM Wanaosomea MA ya Kiswahili

0
Meneja Mkuu wa ALAF Limited, Paul Raj akizungumza kwenye hafla hiyo.

 

Dar es Salaam, 15 Desemba 2022: Kampuni ya mabati ya ALAF Limited leo imetoa ufadhili kwa wanafunzi wa UDSM wanaosomea MA ya Kiswahili katika hafla iliyofanyika chuoni hapo na kuhudhuriwa na wageni mbalimbali wakiwemo wanafunzi waliowahi kunufaika na ufadhili wa kampuni hiyo miaka kadhaa iliyopita.

Akikabidhi ufadhili huo Meneja Mkuu wa ALAF Limited, Paul Raj amesema;

Naibu Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Boniventure Rutinwa alipokuwa akiwapongeza ALAF Limited kwa ufadhili huo na kuwaomba waendelee na moyo huo. 

 

“Awali ya yote ninapenda kutumia fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu muumba wa mbingu na ardhi kwa kutuwezesha kukutana siku ya leo katika tukio hili muhimu.

“Aidha, niwashukuru kwa dhati wadau wetu kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na ninyi wanahabari kwa kuungana nasi katika hafla fupi ya ufadhili wa Kampuni ya ALAF LIMITED kwa wanafunzi wanaosoma MA Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Meneja Mkuu wa ALAF Limited, Paul Raj akimpongeza mmoja wa wanafunzi waliopatiwa ufadhili huo wakati akimpa mfano wa hundi ya fedha za ufadhili huo.

 

“ALAF imekuwa ikijihusisha na utoaji wa Tuzo za Fasihi ya Kiswahili kwa takribani miaka minne şaşa, tangu mwaka 2016, na daima Chuo Kikuu cha Dar es Salaam wamekuwa ni wadau muhimu sana katika mchakato wa utoaji wa tuzo hizo.

“Jambo hili mbali na mambo mengine limelenga kuunga mkono jitihada za serikali ya awamu ya sita katika kuhakikisha kuwa tunakitangaza Kiswahili ndani na nje ya nchi kwani lugha hii ni miongoni mwa tunu za taifa letu na urithi wa pekee tulioachiwa na Baba wa Taifa hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

“Katika kuunga mkono juhudi za serikali na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kampuni ya mabati ya ALAF LIMITED kwa mara ya nne sasa inatoa ufadhili kwa wanafunzi watatu wanaosomea shahada ya Umahiri katika Kiswahili (MA Kiswahili) katika Taasisi ya Taaluma za Kiswahili ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

“Tutaendelea kutoa ufadhili zaidi kwa kadiri hali itakavyoruhusu. “Tunakishukuru kwa dhati Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kupitia Taasisi ya Taaluma za Kiswahili kwa kuridhia nia yetu na kuandaa vigezo vinavyotumika kuwapata wanafunzi hao.

“Chuo hiki kimeonesha imani ya pekee kwetu nasi hatuna budi kukishukuru kwa dhati. “Mkurugenzi wa Taasisi ya Taaluma za Kiswahili atawapatieni taarifa kamili inayoonesha vigezo vilivyotumika katika kuwapata watunukiwa wetu wa ufadhili.

“Pia ninawasihi wale waliofanikiwa kupata ufadhili huu kufanya juhudi katika masomo yao ili kwa pamoja tuweze kukuza na kuendeleza lugha yetu adhimu ya Kiswahili. “Asanteni sana kwa kunisikiliza na kuwa nasi katika tukio hili muhimu”. Alimaliza kusema meneja huyo.

Naye Naibu Makamu Mkuu wa chuo hicho, Boniventure Rutinwa aliishukuru sana ALAF LIMITED kwa ufadhili wao na kuwaomba kuendelea na moyo huo na hata kufikiria kuongeza ufadhili huo kwa wanafunzi wengi zaidi.  HABARI/PICHA NA RICHARD BUKOS /GPL

Leave A Reply