The House of Favourite Newspapers

ALAF Yakabidhi Mabati Yenye Thamani ya Sh 35m kwa MOI

0
Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Limited (Tanzania), Theresia Mmasy (wa tatu kushoto) akikabidhi msaada wa mabati yenye thamani ya milioni 35 kwa Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo, Dk. Antony Assey (wa pili kushoto) ili kusaidia ukarabati wa Kitengo Cha Wagonjwa wa Nje (OPD) na eneo la mapokezi. Wanaoshududia ni watumishi wa MOI na ALAF.

ALAF Limited (Tanzania), moja ya makampuni yanayoongoza katika kutoa suluhisho kwa ujenzi imekabidhi mabati yenye thamani ya Sh35 milioni kwa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) kusaidia mradi wa ukarabati wa taasisi hiyo.

Akikabidhi msaada huo MOI, Ofisa Mawasiliano na Uhusiano wa ALAF Limited Bi. Theresia Mmasy alisema hiyo ni sehemu ya mpango wa kampuni hiyo katika kusaidia jamii.

Alisema msaada huo unalenga kusaidia Taasisi hiyo kufanya ukarabati wa Kitengo Cha wagonjwa wa nje (OPD) na eneo la mapokezi.

“Sisi ni sehemu ya jamii na nia yetu ni kuona watu, ambao pia ni wateja wetu, wanapata huduma bora ambazo zitawezeshwa na ukarabati huu,” alisema.

Bi Theresia aliipongeza MOI kwa kutekeleza mradi huo wa ukarabati ambao utawafanya wagonjwa wengi zaidi kutoka Tanzania nzima kuhudumiwa Kwa haraka.

“Tunaahidi kuendelea kuunga mkono miradi kama hii kwa manufaa ya jamii,” alisema.

Kwa upande wake, Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa MOI, Dk.Antony Assey aliishukuru ALAF Limited kwa mchango wake huo na kusema kwamba utasaidia kwa kiasi kikubwa katika ukarabati huo na kufanya Kitengo cha OPD pamoja na mapokezi kuwa vya kisasa zaidi.

“Msaada huu imekuja wakati mwafaka zaidi kwani utahakikusha tunatoa huduma Bora zaidi mara ukarabati huu ikikamilika,” alisema.

Alitoa wito kwa makampuni mengine na mashirika kuiga mfano wa ALAF.

ALAF Limited ni kampuni inayoongoza nchini Tanzania kwa kutengeneza mabati ya kuezekea nyumba. Ni kampuni iliyoanzishwa mwaka 1960, na inaendelea kuwa mdau muhimu katika maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini.

ALAF imeunganisha kikamilifu operesheni, si tu kwa kutengeneza mabati, lakini pia kwa kuzalisha vifaa vinavyotumika katika shughuli mbalimbali za uezekaji wa nyumba. ALAF Limited hutengeneza vifaa mbalimbali vya metali kwa matumizi mbalimbali ya uezekaji wa nyumba.

www.alaf.co.tz

Leave A Reply