The House of Favourite Newspapers

Albamu Mpya, Harmonize Kuangusha Balaa Mlimani City Leo

0

MSANII wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul Kahali, maarufu kwa jina la Harmonize,  ameweka wazi kuwa anaachia album yake mpya leo Jumamosi, Machi 14, 2020, inayoitwa ‘Afro East’ ambayo  ina ngoma 18.

 

Harmonize amesema kati ya ngoma hizo 18, ngoma 15  ni mpya huku zile tatu zikiwa ni Uno, Hainishtui na Hujanikomoa.

 

Unajua nimejitahidi sana kuhakikisha ngoma nyingi kwenye Afro East zinakuwa mpya, kwa hiyo watu watakaokuja na wale ambao hawatafika watafurahia albam hii wakinunua,” amesema.

 

Kwa watakaohudhuria uzinduzi huo unaofanyika Mlimani City,  amesema mama, baba na mke wake huenda wakawepo kama itampendeza Mungu maana atakuwa pia anasherehekea  bethidei yake na ameahidi itamkuta jukwaani akitumbuiza.

Leave A Reply