Kartra

Albamu ya Kiba Yazidi Kukimbiza

KILA mmoja anafahamu kuwa staa wa Bongo Fleva na CEO wa lebo ya Kings Music Alikiba aliachia album yake tarehe 7/9 mwaka huu inayojulikana kwa jina la THE ONLY ONE KING yenye ngoma 16.

 

Katika ngoma hizo 16 aliachia na video moja ya Oya Oya, album hiyo inaonekana kupokelewa kwa kasi sana na mashabiki wa muziki dunaini kote kwani takwimu zinazidi kuwa kubwa baada ya kuachiwa tu.

 

Zifuatazo ni takwimu za mitandao (Platform) mitatu ya kuuzaia nyimbo ambayo ni Audimack, Spotify na Boomplay. Katika mtandao wa Boomplay tayari album hiyo imefikisha zaidi ya Streaming mil 10.

 

Katika mtandao wa Audimack album hiyo imefikisha Streaming mil 7. Katika mtandao wa Spotify ina straming zaidi ya mil 1.5 mpaka hivi sasa. Huku ikifikisha Streaming zaidi ya mil 18 katika mitandao hiyo mitatu.

Aidha, msanii maarufu wa HipHop @baghdad_pg ameonesha kusikitishwa kukuta Album ya Kiba ikiuzwa mtaani na wauza CD.
Bhagdad ambae ni moja ya viongozi wa moja ya makundi ya wasanii hapa nchini ameeleza kuwa wauza CD hao wanachoma CD kwenye vibanda vya kariako na wanalipia na kisha kuhoji kama serikali imeshindwa kusimamia swala hilo yeye anaweza, anachohitaji ni ruhusa tu.

Toa comment