The House of Favourite Newspapers

Algeria wamvamia Samatta hotelini

0

Samata-vs-MalawiStraika wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.

Nicodemus Jonas na Ibrahim Mussa
ALGERIA wapo juu katika takwimu za ubora wa viwango vya soka lakini hiyo haimaanishi kuwa nao hawana hofu juu ya timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, hiyo ni baada ya mashushushu wa Waarabu hao kuvamia hotelini bila makubaliano na kumtafuta straika wa Taifa Stars, Mbwana Samatta.

Samatta ambaye ameibuka kuwa Mfungaji Bora wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ameonekana kuiteka Afrika, hali ambayo pia inawapa hofu Waalgeria hao, ndiyo maana walipotua Dar tu, mguu wa kwanza ukatua kwa Samatta.

Taifa Stars inatarajiwa kukipiga na Algeria, kesho Jumamosi ikiwa ni mechi ya kuwania kufuzu Kombe la Dunia 2018, ambapo timu hizo zitarudiana katikati ya wiki ijayo nchini Algeria.

FILAMU ILIVYOKUWA:
Samatta na mwenzake, Thomas Ulimwengu ambaye wanacheza wote katika Klabu ya TP Mazembe ya DR Congo, walitua nchini juzi na moja kwa moja wakapelekwa katika Hoteli ya Serena jijini Dar ili kuwasubiri wenzao waliokuwa wakitokea Afrika Kusini.

Jana asubuhi, gazeti hili lilifika hotelini hapo na kuwasiliana na Samatta ambaye alifika mpaka mapokezi kisha kukaa meza moja na kuanza kufunguka mambo mbalimbali.

Wakati mahojiano yakiendelea, ghafla Waarabu watatu waliingia hotelini hapo na kuanza kuzungushazungusha shingo, mara wakamuona Samatta akihojiwa na waandishi wa gazeti hili, mmoja wao akaanza kuzungumza kwa Lugha ya Kiarabu huku akimsonta Samatta, kwa akili ya kawaida ni kama alikuwa anasema: “Huyu hapa…huyu hapa.”

Waarabu hao waliokuwa wameshika vitu kwa kuvificha walianza kama kubishana hivi kama wanayemuona ni Samatta au la, baada ya kugundua kuwa ni yeye, wakafika mpaka eneo alilokuwepo na kuomba kufanya naye mahojiano.

Hata hivyo baada ya waandishi wa Championi kuwabana, walikiri kuwa ni Waalgeria, wawili ni waandishi wa habari na mmoja ni shabiki ambaye huwa anasafiri bure na kuhusika kusoma mazingira ya timu popote inapokwenda.
“Kweli sisi tunatoka Algeria, tumetangulia huku na timu inakuja leo (jana) saa tatu usiku, tumetangulia kwa ajili ya kuangalia mazingira, ndiyo maana tuko hapa,” alisema mmoja wao aliyejitambulisha kwa jina la Ahmed.

“Ni kweli utaratibu upo, lakini tunaomba kidogo tuongee naye, maana tunamjua huyu mtu, juzi alitwaa ubingwa na Mazembe, tunataka walau tuongee naye kidogo hapahapa,” alisema mwandishi aliyejitambulisha kwa jina la Ahmed ambaye alionekana kuwa na mchecheto huku muda wote akichekacheka.

SAMATTA AWACHENJIA, AWAPOTEZA MABOYA
Samatta ambaye ghafla alibadilika sura na kuonekana yupo ‘serious’ alikubali kuhojiwa na Waarabu hao lakini akawapoteza kwenye lugha ambapo walikuwa wakimuuliza kwa Kifaransa yeye akawa anajibu kwa Kiingereza huku akionekana kuwa makini na majibu yake. Zaidi walimhoji juu ya wachezaji anaowajua na jinsi anavyoijua Algeria.

Baadaye Waarabu hao walikiri kufikia hoteli nyingine lakini walifika hapo kwa ajili ya kumuona Samatta. “Tumefikia kwingine, sema tumekuja kuwaona Samatta na mwenzake (Thomas) Ulimwengu,” alisema mmoja wao.

WAIPONDA BEKI STARS, FOWADI HATARI
“Tumewaona (Stars) wako vizuri ila hawana beki. Beki yao ni sifuri kabisa, ila mbele ni hatari sana. Ulimwengu, Samatta safi kabisa.”

Mastaa kibao kuikosa Stars
Aidha, Algeria ilitarajiwa kufikia katika Hoteli ya Kilimanjaro.

SAMATTA AFUNGUKA MBINU CHAFU
Wakati huohuo, Samatta alisema anawajua vema Waarabu na kwamba lazima wawe makini nao. “Nimecheza mara kadhaa na Waarabu, ni hatari sana kwa kuwatoa watu mchezoni. Mchezo wa Jumamosi lazima kuwa makini,” alisema.

Leave A Reply