Ali Kiba akasirishwa wasanii kuhonga kwenye tuzo
Staa anayekimbiza kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’.
BONIPHACE NGUMIJE
SUPA staa anayekimbiza kwenye tasnia ya muziki wa Bongo Fleva, Ally Saleh ‘Ali Kiba’ hivi karibuni amekasirishwa na hatua ya wasanii kutumia pesa ili kujinyakulia tuzo.
Akichonga na Amani, Kiba ambaye kwa sasa anabamba na Ngoma ya Nagharamia aliyoshirikiana na Christian Bella ‘Obama’ alisema kuna baadhi ya wasanii (hakupenda kuwaweka wazi) hutumia pesa ili kujinyakulia tuzo mbalimbali za kimataifa jambo ambalo anadai si sawa.
“Nimegundua kuwepo na baadhi ya wasanii ambao hutumia pesa ili kutangazwa kuwa ni washindi katika baadhi ya tuzo fulanifulani, jambo hilo nimeligundua hivi karibuni na si sawa hata kidogo kufanywa na mtu anayejiita kuwa ana uwezo wa kushindana na wasanii wakali kama mimi,” alisema Kiba.