The House of Favourite Newspapers

Ali Kiba Seduce Me ni Zaidi ya Muziki Mzuri

0

 

Alikiba.

Makala: Hashim Aziz

DO not do like that, I’m too smart dada, seduce me like what the hell (ah hold up), what the hell, don’t do like that, I’m too smart dada, seduce me like what the hell (ah hold up) what the hell…”

Ukisikia kiitikio hicho, basi tambua kitaa kimewaka, watu wanatafutana, Ali Saleh Kiba amekiwasha na sasa mitaa yote inakiri kwamba kweli yeye ni King!

Hiki ni kiitikio cha wimbo mpya wa Ali Kiba, Seduce Me (Kipusa) ambao ndani ya siku chache tangu auachie, ameshakula ‘views’ zaidi ya milioni 2.4 (mpaka leo Jumanne) kwenye Mtandao wa YouTube huku ukiwa gumzo kwenye vituo vya redio, runinga na kwenye mitandao ya kijamii!

Licha ya kuchanganya ung’eng’e kiasi, mantiki ya wimbo huo inaeleweka vyema hata kwa Mtanzania wa kawaida, anaimba mapenzi lakini katika mtindo wa tofauti kidogo. Anamtahadharisha mwanadada ‘anayejigonga’ kwake, kwamba hata kama anampenda na kujitongozesha, anapaswa kuwa makini kwa sababu yeye ni ‘play boy’, mitaa yote inamjua kwa kupenda totoz na kuvunja mioyo ya akina dada!

Hebu msikilize kwenye ‘verse’ ya kwanza anavyotiririka na mistari juu ya ‘melody’ tamu isiyochosha masikioni:

“Nakuona unakata, be carefully sister, na kama unataka, they call me heart breaker (breaker), nina majina mapya, kila mmoja amenipa, wananiita kipusa, ooh pasua kichwa, nina majina mapya, kila kona wamenipa, wananiita kipusa, ooh pasua kichwa!

 King Kiba anamtahadharisha mwanadada huyo anayemzimikia, kwamba japokuwa anaonesha kumpenda kwa dhati, lakini anapaswa kuwa makini kwa sababu mwisho wa yote  tamuumiza tu, hawezi kutulia na mpenzi mmoja, ni hodari wa ‘kupiga na kusepa’ mpaka mitaaniwamemtungia jina la kipusa!

Baada ya verse hii ya kwanza, Kiba anarudia tena chorus, do not do like that, I’m too smart dada, seduce me like what the hell (ah hold up)… kisha anaingiza verse ya pili ambayo kama ile ya kwanza, anaendelea kujinadi kwa mrembo wake, hebu cheki mwenyewe:

“Najua kupenda, nagawa mavumba, na kama unataka, they call me Kiba Rockstar, nina mandinga mapya, kila mmoja nampa, wananiita misifa, ooh pasua kichwa, nina mandinga mapya, kila mmoja nampa, wananiita misifa, ooh pasua kichwa!

 Daah! Siyo kwa kujisifi a huku, Kiba anatamba kwamba kunak malavidavi, anajua haswaa kupenda, mkwanja kwake siyo tatizo, anagawa tu mavumba (fedha) na kama hiyo haitoshi, wadada anaokuwa nao kwenye uhusiano, haoni hatari kuwahonga mandinga (magari), anajinadi kwamba anapenda sifa kwa sana lakini mwisho wa siku, akishapata anachokitaka, akishalikinai penzi, lazima akutende na kukuumiza moyo.

Baada ya verse hii, anaingiza tena chorus halafu kuna ubunifu wa hali ya juu Kiba anauingiza kwenye outro (kipande cha kumalizia), hapa anachanganya fl eva na utasikia ladha fulani ya muziki wa Charanga, ambapo anasikika akitamba:

“Yoop! You know me girl, I go by the name of Alikiba, Unstoppable, Walter Mama lailalaila mama, despacito, despacito, cheza kidogo!

Despacito ni neno la Kispaniola linalomaanisha taratibu, hapa anamhimiza mrembo wake kucheza taratibu kwa madaha!

Kwa wafuatiliaji wa muziki, ukisikia despacito, unaizungumzia ngoma nyingine iitwayo Despacito inayokimbiza kinoma kwa sasa kwenye anga la burudani, ya mkali kutoka nchini Hispania, Luis Fonsi akiwa na Daddy Yankee ambapo katika remix amemshirikisha pia Justin Bieber!

Kwa kifupi, Ali Kiba ameonesha ni kwa namna gani amekomaa kisanii na kwa kiasi kikubwa, ameweza kuikata kiu ya mashabiki wake, waliokuwa wakimsubiri kwa hamu tangu alipotoka na Aje, takribani mwaka mmoja uliopita.

Ukitazama katika kamusi ya Kiswahili, neno kipusa linamaanisha pembe ya faru, bidhaa ambayo inawindwa sana na majangili lakini neno hilo p a hutumika kumaanisha kitu chenye thamani kubwa au kitu kinachopendwa na wengi, awe ni mwanamke mzuri au mwanaume mwenye mvuto.

Kwa jinsi ngoma hii ilivyopangiliwa, kuanzia kwenye mashairi yake, mdundo, melody mpaka video ambayo japokuwa ipo ‘simple’, ina ubora wa kimataifa, Ali Kiba amethibitisha kwamba kweli yeye ni kipusa katika gemu la muziki wa kizazi kipya Bongo!

Leave A Reply