The House of Favourite Newspapers

ALIBIKA AFUNGUKA KWANINI MOFAYA HAIJAINGIA SOKONI

STAA wa Bongo Fleva, Alikiba amefunguka na kueleza sababu za kwanini hadi sasa kinywaji chake cha MoFaya Energy bado hakijaingia sokoni licha ya kukinadi kwa nguvu kubwa kuanzia siku ya harusi yake alipokizindua.

Kiba amesema kila hatua imekamilika ingawa kuna kitu kilikwambisha lakini ana imani siku siyo nyingi kitaingia sikoni.

“Ok, tayari tumemaliza kila process nadhani kuna delay kidogo imetokea ambayo imefanya hadi sasa watu hawaioni katika soko ila bila shaka Mwenyenzi Mungu akijali hivi karibuni itakuwa tayari na ninaomba Watanzania waipokee,” amesema Alikiba.

 

Utakumbuka kinywaji cha MoFaya kilitambulishwa kwa mara ya kwanza April 29, 2018 ambayo ilikuwa siku ya harusi ya Alikiba.

Comments are closed.