Alichokiandika Wema Baada ya Lema Kupata Dhamana
Leo Machi 03, 2017 Wema ameandika ujumbe baada ya Mahakama Kuu Kanda ya Arusha, kutoa dhamana kwa Mbunge wa Arusha Mjini, Godbless Lema (Chadema) aliyewekwa kizuizini kwa takribani miezi minne tangu Novemba 2 mwaka jana alipokamatwa.
Mungu ni mkubwa….Ni furaha kusikia Mh. Godbless Lema amepewa dhamana….Najua ulipita katika wakati mgumu sana, najua ulikuwa mbali na familia yako, watoto wako, rafiki zako, makamanda wenzako na zaidi wananchi wako wa Arusha na Watanzania kwa ujumla….Ni faraja kwetu kwamba sasa umerudi mtaani kuendeleza mapambano…. Kwenye mapambano haya hautakuwa mwenyewe; Mdogo wako Wema nitakuunga mkono mpaka kieleweke….For that sake, Kesho i’ll be in Arusha kuonyesha Solidarity ✌🏼✌🏼✌🏼 “FOR TO BE FREE IS NOT MERELY TO CAST OFF ONE’s CHAINS, BUT TO LIVE IN A WAY THAT RESPECTS AND ENHANCES THE FREEDOM OF OTHERS” – NELSON MANDELA #CallMeKamanda”
Comments are closed.