The House of Favourite Newspapers

Alichokifanya Tido Mhando Baada ya Kuachiwa Huru! – VIDEO

Aliyekuwa Mkurugenzi wa TBC Tido Mhando ameachiwa huru na Mahakama ya hakimu mkazi kisutu na kufutiwa mashtaka yaliyokuwa yanamkabili LIKIWEMO la matumizi mabaya ya madaraka kwa kusaini makubaliano kwa utangazaji wa digital duniani kati ya TBC na BVl.

Tido ameachiwa huru leo Ijumaa Januari 25, 2019 baada ya mahakama hiyo kumkuta hana hatia.

Hukumu hiyo imetolewa leo na Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi baada ya upande wa mashtaka kushindwa kudhibitisha mashtaka yake. Tido alifikishwa Kisutu kwa mara ya kwanza Januari 26, 2018, kujibu mashtaka matano.

Katika kesi hiyo ya uhujumu uchumi namba 7/2018, Tido alikabiliwa na mashtaka matano, mashtaka manne ni ya kutumia madaraka vibaya na moja la kuisababishia Serikali hasara ya Sh887.1 milioni.

Baada ya kuachiwa huru Tido ameonekana kuwa na furaha huku akikumbatiana na ndugu, jamaa na marafiki zake waliofika Mahakamani hapo.

Comments are closed.