Alichokisema JOTI Kuhusu Mzee MAJUTO -Video

Msanii mahiri wa vichekesho nchini, Joti, amesema kuwa Marehemu Mzee Majuto alikuwa akiwasisitiza sana wafanye kazi bila ya kujivuna na kudharau watu wengine.

 

Mzee Majuto alifariki usiku wa Jumatano, Agosti 8, 2018 katika Hospitali ya Muhimbili, ambapo kesho yake, Agosti 9, 2018 mwili wake ulitolewa na kupelekwa katika Msikiti wa Maamur, Upanga jijini Dar es Salaam kuswaliwa kabla ya kupelekwa Karimjee kuagwa.

 

Baadaye mwili huo ulisafirishwa kuelekea jijini Tanga, ambako atapumzishwa na kuhitimisha safari yake hapa duniani. Marehemu ameacha mjane na watoto kumi. Innah Lillah Wainna Ilaih Rajiun.

Loading...


Stori zinazo husiana na ulizosoma

Toa comment